25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Waandishi watakiwa kusoma muswada wa habari

deogratius-nsokoloNa CLARA MATIMO- MWANZA

WAANDISHI wa habari wametakiwa kuusoma na kuuelewa vyema muswada wa sheria ya huduma za habari wa  mwaka 2016, uliowasilishwa bungeni na Serikali.

Wito huo ulitolewa jijini hapa juzi na Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deogratius  Nsokolo, wakati akifungua  mkutano mkuu wa dharura wa wanachama wa muungano huo uliokuwa na lengo la kujadili na kupitisha mpango mkakati wa mwaka 2016/2020.

Nsokolo alisema endapo waandishi wa habari watausoma muswada huo na kuuelewa na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kutoa maoni, utasaidia  kutungwa sheria bora itakayokuwa na masilahi katika sekta ya habari.

“Tambueni kwamba ili muweze kutoa maoni bora yatakayotumika kutunga  sheria ambayo itagusa tasnia yetu ya habari inayoweza kutumika kwa zaidi ya miaka 50, ni lazima muusome na kuuelewa vyema muswada huo, hivyo nawasihi ndugu zangu msifanye masihara juu ya hili, inatakiwa sisi waandishi tushiriki kwa asilimia 100,” alisema Nsokolo.

Alisema waandishi wa habari wanaweza kushiriki kutoa maoni yao kupitia klabu zao zilizopo mikoa yote hapa nchini ili kuhakikisha yanafika sehemu husika na yanafanyiwa kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles