25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

January: polisi waliniita kunihoji kuhusu Mo, sikukamatwa

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba, amesema hakukamatwa na polisi akihusishwa na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo) kama inavyodaiwa isipokuwa kuhojiwa kama rafiki wa mfanyabiashara huyo.

Amesema polisi wamemhoji kama kuna chochote cha ziada kuhusu mfanyabiashara huyo ambacho amemueleza na kinaweza kusaidia uchunguzi.

Inadaiwa January alikamatwa na polisi na kuhojiwa kwa saa kadhaa, pia Jeshi la Polisi limethibitisha kumhoji waziri huyo lakini hata hivyo, baada ya kuhojiwa na polisi January aliandika katika ukurasa wake wa Twitter akisema; “sijakamatwa na polisi. Niko salama.”

Hali hiyo ilizua mjadala kwa wafuasi wake katika mtandao huo wa Twitter na mitandao mingine ya kijamii wakihoji ni kwanini anasema hajakamatwa na polisi wakati jeshi hilo limethibitisha na kwamba wanaokamatwa na polisi huwa hawako salama.

January katika hatua nyingine amezua sintofahamu baada ya kuandika tena katika ukurasa wake huo huo wa Twitter; “Ufafanuzi: polisi walinipigia simu kuniomba, kama rafiki wa @moodewji, niwasaidie kama kuna chochote cha ziada ambacho Mo aliniambia kinachoweza kusaidia uchunguzi.

“Niliwaeleza. Wakasema kinafanana na alichowaeleza. Wakanishukuru. Wamefanya hivi pia kwa wanafamilia. Sikukamatwa,”.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles