28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Jack Simela, wenzake watano wazikwa Morogoro


Mwandishi Wetu , Morogoro
Mwanamuziki wa  Mchiriki kutoka kundi la Jagwa Music, Jackson Kazimoto maarufu Jack Simela amezikwa leo Desemba 10, katika makaburi ya Bigwa mkoani Morogoro.


Jack amezikwa katika makaburi hayo pamoja na mjomba wake, Ibrahim Karata ambaye ni mtoto wa shangazi yake, Elizabeth Kazimoto aliyezikwa jana katika makaburini hapo.


Baba wa msanii huyo, Leonard Kazimoto ameiambia Mtanzania Digital kuwa msanii huyo, mjomba wake na wenzake watano walifariki dunia wakiwa njiani kwenda makaburi ya bigwa kwa mazishi ya shangazi wa msanii huyo.


“Wakati tunaenda kuzika tulitoka wote hapa maana msiba ulikuwa Mwembesongo wao walikuwa saba wote waliingia kwenye gari lao dogo walipitia barabara kuu ya Moro/ Dar sisi tulipita barabara ya zamani ya Dar, tulipofika makaburini ilituchukua muda kuwasubiri maana tulitaka Jack amzike shangazi yake na pia Ibrahimu Karata naye amzike mama yake ila tulipoona hawatokei tukazika.


“Kumbe walikuwa wamepata ajali eneo la nane nane maarufu kwa jina la Jordan na wote sita wamefariki dunia isipokuwa mmoja amelazwa yupo hoi hospitalini,’’ amesema.


 Amesema waliporudi nyumbani walishangaa kuona vilio vikizidi walipohoji ndipo wakaambiwa kuna msiba mwingine Jack, Ibrahim na wenzao wengine waliokuwa kwenye gari ndogo waligongana na gari kubwa.


Naye shangazi wa msanii huyo, Yasinta Kazimoto amesema alimlea msanii huyo aliyezaliwa 1986 tangu alipokuwa na miaka nane baada ya mama yake mzazi kufariki mwaka 1994.


“Nilimlea vizuri hadi mwaka 2004, alipokuja kuchukuliwa na meneja wake, Gola tangu alipomuona alipokuwa akiimba kwenye moja ya maonyesho ya Jagwa Manzese mkoani hapa hadi sasa mauti yemamkuta ameishi katika kundi la Jagwa kwa miaka 13, alikuwa mtu safi alinipa zawadi kila aliposafiri sikupata naye tabu katika malezi yake,’’ amesema Shangazi yake.


Ameongeza kwamba msanii huyo ameacha watoto watatu, Saidi (18), Nuru (17) na Leonard (4).


Meneja wa mwanamuziki huyo, Abdallah Salehe maarufu meneja Gola amesema kifo cha msanii huyo aliyehitimu elimu ya msingi Shule ya Mwembesongo mkoani hapa ni pigo kubwa kwa tasnia ya muziki wa mchiriku na kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa amebaki kuubeba muziki huo.


“Jack ndiye alikuwa amebaki kuubeba muziki wa mchiriku kifo chake ni pigo kubwa kwa muziki huo, kwani uwezo na uvumilivu wake baada ya wasanii wengi kuliacha kundi la Jagwa ndiyo ulikuwa ukibeba kundi hilo kote ndani na nje ya nchi walipokuwa wakifanya maonyesho yao,’’ amesema Gola.


Hata hivyo baadhi ya wasanii ambao hawakutaka kutajwa majina yao walishangazwa na wadau wa muziki huo kutokufika katika mazishi ya msanii huyo huku wakiongeza kuwa wajenge utamaduni wa kuzikana, sababu wote njia yao ni moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles