28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Magufuli ‘awabipu’ wafanyabiashara wakwepa kodi

AnnaPotinus, Dar es Salaam

Rais John Magufuli, ameibuka na majina yawafanyabiashara wakubwa wanaokwepa kodi nchini ambao ni maarufu kwa kuleta bidhaa na kusambaza kwa wafanyabiashara wengine.

Ameyataja majina ya wafanyabiashara hao kwa namna yake ambapo mmoja amemtaja kwa neno moja na mwingine kwa herufi ya mwisho.

Tukio hilo limetokea leo Jumatatu Desemba 10, ambapo Rais Magufuli alikuwa katika kikao maalumu kati yake uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kilichofanyika jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambome ngine ameitaka TRA kuendelea kutoa adhabu kwa wakwepa kodi.

“Sitaki kuwataja majina wale ambao ni maarufu kwa kuleta bidhaa mmoja anaishia na neno Agency na mwingine anaishia na O mwisho.

“Pia kuna mtu mmoja mkoani Mwanza anaweza kupitisha magari hata 10 na anapopeleka bidhaa zake anauza kwa bei ya chini maana hajalipa kodi na anashirikiana na maofisa wa TRA.

“Biashara ya Kariakoo inajulikana wapo matajiri wawili wanaoleta makontena hata 700 kwa mwaka na wakishawauzia wanakua wanatoa bidhaa kidogo kidogo wakati wana uwezo wa kuagiza hizo bidhaa wenyewe halafu TRA hawajui,” amesema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles