KUNDI la muziki wa kizazi kipya la Jicho Angavu Crew (JAC) la Arusha linatarajiwa kunogesha onyesho la kuzuia mauaji ya albino litakalofanyika Machi 12 katika ukumbi wa UAACC, Maji ya Chai, Arusha.
Katika onyesho hilo, kundi hilo linaloundwa na vijana wanne, akiwemo kiongozi wao, Chediel Greyson ‘Pyda’, Emanuel Greyson ‘Ramsee’, Oscar John ‘Okadi’ na Fyakryus Otto ‘Days’ limeandaa wimbo wa pamoja kuhusu kupinga mauaji ya albino.
“Tumejipanga kutoa hamasa kwa wanajamii kuachana na mauaji ya ndugu zetu albino kwa kuwa kila binadamu yupo kwa sababu za Mungu,’’ alisema Ramsee.
Pia kundi hilo limewataka mashabiki wao wajitokeze kwa wingi ili kupokea ujumbe na onyesho waliloandaa kwa ajili yao.