23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Madam Ritha: Wasanii tumieni fursa ya ving’amuzi

MADAM RITHA...NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI wa Kampuni ya upigaji picha za video ya Benchi Mark Production, Ritha Paulsen, amewataka wasanii watumie fursa ya wingi wa ving’amuzi na vyombo vya habari kwa kuzalisha bidhaa bora na za nyumbani.

Ritha alisema kutokana na wingi wa ving’amuzi kwa sasa, uhitaji wa vipindi vya nyumbani ni mkubwa, hivyo wasanii na maprodyuza wa video wanatakiwa kutumia fursa hizo ili kujipatia fedha na kukuza uchumi wao.

“Huu ni muda muafaka kwa wasanii wa ndani kufanya  ‘production’, kwa kuwa ving’amuzi vipo vya kutosha na vituo vya runinga vinatafuta ‘local content’,’’ alieleza Madam Ritha.

Katika hatua nyingine, msanii anayetamba na wimbo wa ‘Katoto’, Kayumba Juma, amemshukuru Madam Ritha na kampuni yake kwa kufanikisha video ya wimbo wake huo kama walivyokubaliana awali.

“Kulikuwa na mikataba lakini nashukuru wamenifanyia kazi yangu ambayo kwa sasa napita nayo kifua mbele na naamini itaniweka sehemu nyingine na kazi yote hiyo amefanya Madam Ritha na sasa kazi zangu zinasimamiwa na Mkubwa Fella, ambaye anahakikisha najulikana na nyimbo zangu zinafika mbali,’’ alieleza Kayumba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles