22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Izzo Business kuachia Kidawa

izzoNA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Emmanuel Simwinga ‘Izzo Business’, leo anatarajia kuachia video na audio yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Kidawa’ akiwa amemshirikisha mwanadada, Sarah Kaisi ‘Shaa’.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Izzo B alisema kazi yake mpya imetengenezwa na Prodyusa Dupy (video) na mkongwe Master J kwa upande wa audio, huku akiamini ya kuwa video hiyo itakuwa na ubora zaidi.

“Kama unavyojua kila siku zinavyokwenda kiwango kinazidi kuongezeka, hivyo nina imani video yangu itakuwa nzuri zaidi na naamini mashabiki wataipokea vizuri kutokana na ubora wa hali ya juu na kazi nzuri niliyoifanya itakayowashika mashabiki wangu na Watanzania kwa ujumla,” alisema.
Izzo Business amewahi kutamba na nyimbo kadhaa ikiwemo Tumogele, Haina Kufeli, Love Me, hivyo amewataka mashabiki wakae mkao wa kula wa kupokea nyimbo kali mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles