22.7 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Izzo Bizness ashangazwa na ‘surprise’ ya uongozi wake

IzzooooNA SUZANA MAKORONGO (RCT)

MSANII wa Bongo Fleva nchini, Emanuel Simwinga ‘Izzo Bizness’, ameweka wazi kwamba hatozungumzia ujio wake mpya kwa kuwa hajui uongozi wake utachagua wimbo gani wa kutoa kutoka katika albamu yake ya nyimbo 20.

Albamu hiyo itakuwa ya kushangaza kwa kuwa haijulikani siku ya kutoka kiasi kwamba inamchanganya msanii huyo kuanza kuzungumzia ujio wake huo mpya.

“Ujio wangu mpya utakuwa wa ‘surprise’ kwa sababu sijui uongozi wangu utachagua wimbo gani wa kuutoa kabla ya albamu ya nyimbo 20 lakini nina hakika ujio huo utakuwa wa mafanikio kwangu na wanaopenda muziki wangu,” alisema Izzo.

Katika hatua nyingine mkali huyo wa hip hop alipongeza wasanii wanaopiga picha za video za nyimbo zao nje ya nchi kwa kuwa zinakuza muziki wa Afrika kwa kasi na kuitambulisha Tanzania nje.

“Kufanya muziki nje ya nchi ni kawaida na nzuri kwa wasanii wetu kwa kuwa wanatangaza nchi na pia inakuza muziki wa Afrika kwa ujumla,” alimaliza Izzo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles