21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Italia yaitengea Tanzania euro 1,250,000

Na Mwandishi wetu

Serikali ya Italia kutenga kiasi cha Euro 1,250,000 za msaada  kwa ajili mahitaji na vipaumbele vya Tanzania katika sekta ya afya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ujumbe wa wataalam wa afya kutoka nchini Italia umewasili nchini leo  Agosti 03, kwa ziara maalum ya kutathimini na kufahamu mahitaji na vipaumbele vya Tanzania katika sekta ya afya kwa hospitali zilizopo nchini.

Ujumbe wa madaktari watatu  utafanya ziara kuanzia leo Agosti 03 – 12, 2021 ambapo utakutana Uongozi wa Wizara ya Afya na kuainisha mahitaji na viapumbele vitakavyoweza kufadhiliwa kwa fedha hizo katika sekta ya afya.

Taarifa hiyo imesema, ujumbe huo unaongozwa na Dk. Davide Bonechi, Dk. Giulia Dagliana na Dk. Beatrice Borchi, ambao wote ni madaktari kutoka kituo cha Taifa la Italia cha Afya Duniani.

Tanzania imekuwa ikishirikiana na Italia katika miradi mbalimbali ya afya hapa nchini ambapo ushirikiano rasmi katika sekta ya afya ulianza mwaka 1968 kupitia Shirika la Madaktari wa Italia-CUAMM-Doctors with Africa.

“Kuanzia wakati huo, Serikali ya Italia imekuwa ikifadhili miradi mbalimbali ya afya kama vile miradi ya kupambana na utapiamlo, afya ya watoto wachanga, afya ya uzazi na kupunguza maambizi ya virusi vya ukimwi,”

“Aidha, Serikali ya Italia imefadhili miradi ya usafi wa mazingira jijini Dodoma katika kuunga mkono jitihada za serikali za utoaji wa huduma za afya, imekuwa ya kwanza kufungua Kituo cha Tiba ya Mifupa na Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Kuambukiza katika Hospitali ya St. Gaspar, Dodoma. Vituo hivyo, vinaendelea kutoa mchango mkubwa katika kuboresha afya ya wananchi wa Tanzania hususan wakazi wa Dodoma,” imesema taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles