24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

UNWTO kuwajengea uwezo wadau wa utalii Tanzania

NA MWANDISHI WETU, KISIWA CHA SAL-CAPE VERDE

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masula ya Utalii Duniani  (UNWTO), limeahidi kushirikiana na Tanzania katika kuweka mikakati bora ya kuwajengea uwezo  watu wa sekta ya utalii nchini kuanzia Juni 2022.

Hatua hiyo inatokana na  hali mbaya ya ugonjwa wa COVID 19  kuidhoofisha sekta ya utalii nchini na Duniani kwa ujumla huku  Jumuiya ya Afrika Mashariki ( EAC) ikikadiliwa kupata hasara ya dola 4.8 bilioni za Marekani ( zaidi ya sh. trioni 11) kwenye sekta ya utalii kutokana na janga la  Corona huku watu milioni 21 wakikosa ajira

Akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro katika kikao cha pembeni mwa mkutano wa UNWTO  wa 64 wa Kanda ya Africa ukilenga kufungua fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii hasa kipindi ambacho  hiyo inachechemea kutokana na ugonjwa wa Corona.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo  unaongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ndumbaro  akiwa na Maofisa na Makamishna Uhifadhi kutoka TFS na TAWA, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Samuel Shelukindo.

Mkutano huo wa UNWTO wa 64 wa Kanda ya Afrika unafanyika kwa muda wa siku nne kuanzia jana  katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde ambapo umewakutanisha mawaziri 30 wa utalii Barani Afrika ukilenga kujadili mustakabali wa utalii barani

Afrika na Duniani kwa ujumla  kutokana na uwepo wa janga la Corona.

Dk. Ndumbaro amemualika Katibu Mkuu wa UNWTO,  Zurabu Pololikashvil kutembelea vivutio vilivyopo Tanzania  na kusisitiza kuwa ataambatana naye katika ziara hiyo.

Hata hivyo, Dk.Ndumbaro amemueleza Katibu Mkuu huyo kuwa Tanzania ni nchi ya kwanza Afrika kwa kufanya vizuri katika  shughuli za Uhifadhi lakini  katika suala la kujitangaza na kutafuta masoko ya utalii imekuwa haifanyi vizuri hivyo ujio wa mafunzo hayo yataiwezesha Tanzania kufanya vizuri katika nyanja hiyo.

Naye Katibu Mkuu wa UNWTO, Pololiskashvil, amesema mafunzo hayo yatatolewa kwa wadau wa utalii ili kuendana na janga la Corona katika kuendesha shughuli za utalii nchini

Amesema mafunzo hayo yatazilenga jamii zinazozunguka vivutio vya utalii ili kuzijengea uwezo wa kushiriki moja kwa moja katika shughuli za  utalii nchini likiwa lengo ni kutengeneza ajira nyingi zaidi kupitia sekta hiyo.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu huyo amemueleza Dk.Ndumbaro kuwa UNWTO  iko mbioni kuandaa kalenda  ya mwaka ambapo Tanzania nayo itakuwepo katika orodha hiyo ya  kuendana na matukio yatakavyopangwa katika mkutano huo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles