KOKU DAVID-DAR ES SALAAM
Chuo cha Kodi nchini (ITA), kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Misaada la Japan (JICA), mwishoni mwa wiki iliyopita wameendesha mafunzo ya utozaji wa kodi katika sekta ya ujezi kwa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Naibu Mkuu wa Chuo cha ITA, Dk Lewis Ishemoi amesema mafunzo hayo ni muendelezo wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa TRA katika ukusanyaji wa kodi katika sekta maalum za Ujenzi, mawasiliano, madini, mafuta na gesi ambazo zinakua kwa kasi.
Amesema mafunzo hayo yataisaidia TRA kuwa na wataalamu waliobobea katika ukusanyaji wa kodi pamoja na kuongeza makusanyo hasa katika sekta ya ujenzi ikiwa ni pamoja na kuuelewa mfumo mzima wa ujenzi, kufahamu mnyororo wa thamani pamoja na wadau wakuu katika shughuli za ujenzi.