24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Milioni 969 zakarabati shule kongwe Tanga

Mwandishi wetu

Serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 969 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya shule ya sekondari Galanos iliyopo mkoani Tanga.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknlolojia William Ole Nasha alipotembelea shule hiyo kukagua maendeleo ya ukarabati wa miundombinu amesema fedha hizo zimetolewa kupitia mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) katika mpango unaolenga  kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika shule hiyo kongwe.

Amesema fedha hizo ni sehemu ya fedha zilizopelekwa katika shule kongwe nchini ambazo zinafanyiwa ukarabati mkubwa lengo likiwa ni kuzirudisha katika hadhi yake ya awali ili ziwe na mazingira mazuri yanayomwezesha mwanafunzi kujifunza na kufaulu vizuri

Katika hatua nyingine, amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Daudi Mayeji  kufuatilia kwa karibu sababu zilizopelekea kukiukwa kwa masharti ya mkataba wa muongozo wa ukadiriaji  majenzi (BOQ), ambao ulielekeza kuwekwa chuma katika varanda za madarasa zinazoruhusu hewa na badala yake yamewekwa matofali ya kuchoma.

“Galanos tumeleta fedha zaidi ya shilingi milioni 696 kwa ajali ya kukarabati miundombinu, baada ya kukagua maendeleo ya ukarabati nimegundua kuna mapungufu makubwa ya kimakusudi, mfano  kwenye madarasa kulitakiwa kuwekwe chuma lakini badala ya kuweka chuma wameweka matofali ya kuchoma bila hata kufuata taratibu wa kufanya mabadiliko” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles