YERUSALEM, ISRAEL
BUNGE la Israel limeridhia muswada wa kwanza wa sheria, ambayo itaweka kikomo cha adhana – wito kwa Waislamu kwenda misikitini kutekeleza ibada ya sala.
Aidha unapiga marufuku matumizi ya vipaza sauti wakati wowote.
Hata hivyo, muswada wa sheria hiyo ulisababisha hasira kubwa miongoni mwa wabunge kutoka jamii ya Waarabu nchini hapa.
Muswada wa kwanza wa sheria hiyo unataka marufuku kwa mwadhini kutumia kipaza sauti kati ya saa tano usiku na saa moja asubuhi, ukilenga adhana kwa sala ya Alfajiri.
Mbali na muswada huo, mwingine unapendekeza marufuku kwa mwadhini kutumia kipaza sauti katika mitaa yenye makazi ya watu, na faini ya kiasi cha euro 2,600 itatozwa kwa yeyote atakayekiuka sheria hiyo.
Sheria ya kwanza itahusu misikiti katika eneo la Jerusalem Mashariki linalokaliwa na Israel na pia maeneo yote ya nchi hiyo, lakini haigusi viwanja vinavyouzunguka msikiti wa al-Aqsa ambavyo vimo katika mgogoro huo.