30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

IRAN YAZIGOMBANISHA MOROCCO, ALGERIA

RABAT, MOROCCO


WIZARA ya Mambo ya Nje ya Morocco imeituhumu Algeria kwa kuisaidia Iran kuwaunga mkono Polisario, vuguvugu linalopigania uhuru wa Sahara Magharibi, eneo ambalo Morocco inasisitiza ni sehemu yake.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco, Nasser Bourita aliliambia jarida la Kifaransa la Jeune Afrique katika mahojiano maalumu kuwa Algeria ilitoa ofa ya mahali pa mkutano kwa Polisario Front na kundi la wanamgambo wa Hezbollah la Lebabon.

Rabat inaituhumu Iran kulitumia kulitumia kundi hilo la madhehebu ya Shia kuunga mkono vuguvugu hilo la waasi wa Sahara Magharibi wanaopambana na Morocco kwa miaka mingi sasa.

“Algeria imetoa baraka zake. Imefungua milango kwa Iran ili kulisaidia vuguvugu hili,” Bourita alisema.

“Hali kadhalika, baadhi ya mikutano baina ya Polisario na Hezbollah ilifanyika kwa siri katika maficho mjini Algiers likimtumia mwanamke wa Algeria aliyeolewa na kada wa Hezbollah, ambaye anatumika kama kiunganishi kati ya kundi hilo na Polisario,” Bourita aliongeza.

Mapema mwezi huu, Morocco ilivunja uhusiano wake wa kibalozi na Iran ikiituhumu kulisaidia Polisario kupitia mshirika wake Hezbollah na kwa uratibu wa ubalozi wa Iran mjini Algiers.

Algiers ilimlima barua balozi wa Morocco nchini humo wakati huo kupinga tuhuma za ufalme huo kwamba inashirikiana na Iran kuliunga mkono vuguvugu hilo la waasi.

Bourita aliongeza kuwa anaamini Algeria inatumia mbinu ikiwamo kuliunga mkono Polisario, ili kupoteza mwelekeo wa mtazamo wa sasa wa matatizo makubwa yanayoikabili nchi hiyo kitaasisi, kisiasa, kiuchumi na kijamii.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles