29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

ACT WAITAKA SERIKALI IBADILI MFUMO WA MIKOPO

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM


CHAMA Cha ACT- Wazalendo kimeishauri serikali kubadilisha mfumo wa utoaji wa mikopo ya elimu ya juu kutoka katika mikopo na kuingia katika mfumo wa ufadhili.

Kauli ya ACT imekuja siku chache baada ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kutoa mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka 2018/19.

Katika mwongozo huo kuna kipengele kinachozuia kuomba mkopo wanafunzi ambao wazazi wao wanamiliki biashara au Meneja wa taasisi yoyote inayotambulika.

Akizungumza na wandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT, Likapo Likapo alisema kipengele hicho kitazalisha matabaka katika jamii kwa kuwatenga watoto wa wafanyabiashara.

“Kipengele hiki kinamaanisha kuwa mtu yeyote atakayesajili biashara yake Brela na TRA hata ya kunyoa tu mwanawe hatapata mkopo wa elimu juu jambo ambalo litazua hofu kwa wafanyabiashara,” alisema Likapo.

Alisema kipengele hicho kitawatia hofu wafanyabiashara kusajili biashara zao kwa hofu ya watoto wao kutokupata mkopo wa elimu ya juu.

“Hili litapunguza morali ya wafanyabiashara kulipa kodi kwa kuwa wakisajili biashara zao watatakiwa kuwalipia masomo ya juu watoto wao,” alisema Likapo.

Aliongeza kuwa hakuna sheria inayowataka wazazi wanaopeleka watoto wao katika shule binafsi kulazimika kusomesha bila ya kulipiwa mikopo ya elimu ya juu.

Aliongeza kuwa ni vema serikali ikafadhili masomo na malazi kwa wanafunzi na kama kuna mwanafunzi atahitaji fedha za kujikimu atalazimika kwenda kukopa katika taasisi za fedha.

Akizungumzia kuhusu kauli ya Rais Dk. John Magufuli kuhusu kufanya siasa vyuoni, Likapo alisema kauli hiyo itawaondolea vijana kujiamini na hivyo kuwa na kizazi cha watu waoga na wasiojiamini.

 

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles