31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

WATU 26 WAUAWA KATIKA SHAMBULIO BURUNDI

BUNJUMBURA, BURUNDI


SERIKALI ya Burundi inasema kuwa watu 26 wameuawa wakati wa shambulio kaskazini magharibi mwa taifa hili.

Mashambulizo hayo yanajiri siku kadhaa kabla ya kufanyika kura ya maoni iliyokumbwa na utata, ambayo huenda ikaongeza muda wa utawala wa rais wa taifa hili.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Waziri wa Usalama Burundi, Alain Guillaume Bunyoni alisema wale waliotekeleza shambulio hilo walikuwa ni magaidi kutoka nchini jirani ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo (DRC).

Amesema baadhi ya waathirika waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini kwa matibabu.

Ameongezea kuwa mazungumzo yanaendelea na mamlaka ya DRC kwa lengo la kuwakamata washukiwa wa shambuilio hilo.

Walioshuhudia wanasema kuwa washambuliaji hao waliingia nyumba baada ya nyumba usiku wakiwapiga risasi watu na kuwachoma visu kisha kuziteketeza moto nyumba zao.

Kuna uwezekano shambulio hilo ni jaribio la kuvuruga kura ya maoni yenye utata iliyopangiwa kufanyika wiki ijayo.

Mchakato huo ni mradi wa serikali unaoweza kumfanya Rais Pierre Nkurunziza kusalia madarakani hadi mwaka 2034.

Kitendo hicho kinapingwa na makundi ya upinzani yakiwamo yaliyofikia makubaliano ya amani ya Burundi mwongo uliopita.

Huenda mgogoro wa kisiasa nchini humo ukachukua mwelekeo mpya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles