24.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Infinix yazindua Note 40 Series

*Teknolojia ya kuchaji haraka kuwapa suluhu watumiaji

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni maarufu ya simu za mkononi, Infinix, kwa ushirikiano na kampuni ya Mawasiliano, Vodacom Plc na Shirika la ndege la Tanzania, Air Tanzania (ATCL) zimelifikisha sokoni toleo la simu mpya ya Infinix NOTE 40 na NOTE 40 Pro.

Kwa mujibu wa taarifa ya Infinix iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam, simu za NOTE 40 na NOTE 40 Pro zinapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania zikiwa na ofa ya GB 96 za internet kutoka Vodacom Plc pamoja na ofa kabambe ya ticket za usafiri wa ndege ya Air Tanzania nje na ndani ya nchi.

“Lengo la Infinix ni kufikia wateja wake kwa ukaribu na kuwaongeza thamani kupitia simu za Infinix, NOTE 40 series zinatizamiwa kuja kupunguza kero kwa watumiaji wa simu janja inapokuja kwenye swala la Chaji.

“Teknolojia ya All Round FastCharge 2.0 yenye Watt 70, Magnetic wireless Charge ya Watt 20 na Cheetah X1 zinaondoa vizuizi vya kuchaji katika hali yoyote na katika hali ya hewa yoyote, simu zetu zinapokea chaji kwenye maeneo ya hali baridi ya hadi nyuzi -20C pia tumeongeza ubora kwenye kamera zetu na muundo wa simu.

“NOTE 40 series ina umbo la muundo wa 3D curved, AMOLED Display, refresh rate 120Hz na Camera ya Megapixel 108 OIS Super- Zoom cam,” amesema Aisha Karupa, Afisa Mahusiano Infinix Tanzania.

Aisha ameongeza kuwa: “Pamoja na uzinduzi wa NOTE 40 series pia tunatambulisha vipuli vya simu ‘SMART WATCH, EARPADS’ pamoja na laptop ambazo zinategemewa kuingia sokoni hivi punde, tunaomba watanzania mtupokee tena kama ambavyo mmezipokea simu zetu na kutufanya kuwa namba moja katika soko letu la simu hapa nchini,” alimaza.

Upande wake Afisa Mahusino Vodacom Plc, Alex Bitegeye alisema kuwa, “Mteja akinunua simu hii aina ya lnfinix Note 40 series ambazo zinapatikana katika maduka yetu makubwa nchini lakini pia katika maduka ya lnfinix, sisi Vodacom tunampa mteja huyu GB 8 kwa mwezi, na hivyo kufanya mteja atakayenunua simu kupata jumla ya GB 96 kwa mwaka mzima.

“Sote tunafahamu kwamba kwa sasa simu sio anasa, bali ni kitu cha muhimu sana kuwa nacho, mbali na kuitumia kama chombo cha mawasiliano lakini mtu anaweza kuitumia kama kitendea kazi.

“Nikisema kitendea kazi namaanisha mtu anaweza kufanya biashara kwa kutumia simu yake ya mkononi, unapokuwa na intaneti madhubuti, basi unaweza kufanya biashara mtandao,” amesema Bitegeye.

Infinix pia imeshirikiana na Kampuni ya ukopeshaji ya Easybuy ambapo mteja anaweza kukopa simu hii kwa kutanguliza asilimia 30 ya bei ya simu kulingana na duka atakalo nunulia, pia washirika wao wa muda mrefu Carl care wenye kujihusisha na utengeneza wametoa offa ya utengenezaji endapo simu itavunjika kioo kwa siku 180 tangu mteja alipoinunua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles