Na MWANDISHI WETU
SHIRIKA la Fedha Duniani (IMF) limesema idadi ya watu nchini inatarajia kuongezeka katika miongo miwili ijayo.
Limeishauri Serikali kujiandaa kwa kutengeneza mazingira mazuri ya ajira.
Hayo yalielezwa na ujumbe wa shirika hilo uliokuwa ukiongozwa na Mauricio Villafuerte, ambao umekuwapo nchini tangu Novemba 30 hadi Desemba 12 mwaka huu.
Lengo la ujumbe huo lilikuwa kupitia sera mbalimbali za uchumi na kuangalia mwenendo wa uchumi kabla ya kutoa ushauri kwa Serikali kufuatana na mpango unaojulikana kama Policy Support Instrument (PSI).
Taarifa iliyotolewa baada ya kumaliza shughuli zake, ilisema Tanzania bado inakabiliwa na changamoto nyingi katika kutekeleza malengo yake ya maendeleo.
Waliitaka Serikali kufanyia kazi changamoto hizo ikiwamo kuimarisha mazingira ya kufanya kazi kwa sekta binafsi.
“Wakati idadi ya watu ikitarajiwa kongezeka katika kipindi cha miaka 20 ijayo, kuandaa mazingira bora kwa ajili ya sekta binafsi kutengeneza ajira, ni jambo la kipaumbele.
“Kuboresha mazingira ya biashara, kuwa na sera zinazotabirika ambazo zinajali maoni kutoka sekta binafsi, maboresho kwenye sera za udhibiti na kurudisha kodi kama VAT na nyinginezo kwa muda muafaka na kulipa madeni ya ndani, ni baadhi ya mambo yanayotakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo inasema takwimu zilizotolewa na mamlaka za Tanzania mwanzoni mwa mwaka 2017, zinaonyesha ukuaji wa uchumi wa aslimia 6.8.
Hata hivyo, taarifa hiyo iliitaka Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) kuangalia upya vyanzo na utaratibu wake wa kuandaa takwimu zinazoeleza ukuaji wa uchumi……….
Kwa habari zaidi pata nakala yako ya MTANZANIA.