28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘Imba Together Live Gospel Event’ kutikisa North Carolina Julai 23

Na Christopher Msekena, Mtanzania Digital

WAIMBAJI maarufu wa muziki Tanzania wanatarajiwa kuungana na waimbaji wengine nchini Marekani katika tamasha la Imba Together Live Gospel Event litakalofanyika mjini North Carolina, July 23, mwaka juu.

Kutoka Tanzania waimbaji watakaopamba jukwaa hilo la kusifu na kuabudu ni Boaz Danken, Dr. Upyana, Joel Lwaga, Goodluck Gozbert, Rehema Semfukwe na Gloria Muliro kutoka Kenya.

Waimbaji hao wataungana na wenzao kutoka Marekani ambao ni
Leonard Mbwambo, Edna Matinde, Colin Allured, Kelly Herton, Brett Anderson na Mett Moger huku lengo kikiwa ni kumsifu na kumwabudu Mungu pamoja na kuongeza uelewa juu ya watoto wenye autism (autizimu) duniani kote.

Aidha tukio hilo litapambwa na mchekeshaji na mchungaji kutoka Tanzania Masanja Mkandamizaji huku Dancer Group kutoka Atlanta watasha moto katika mji wa Calorina kuanzia saa 11 jioni mpaka saa 4 usiku huku kukiwa hakuna kiingilio na chakula ni bure.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles