28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

IGP: Uchaguzi Serikali za Mitaa utakuwa tulivu

Allan Vicent -Tabora

JESHI la Polisi limewahakikishia wananchi kuwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba, utafanyika kwa amani na utulivu.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro alipoongea na wananchi wa Kata ya Kanyenye, Manispaa ya Tabora hivi karibuni.

IGP Sirro alisema uchaguzi ujao ni muhimu  kwa sababu wananchi watapata fursa ya kuchagua viongozi wao wa ngazi za mitaa.

Alisema uchaguzi huo ni wa Watanzania wote na vyama vyote, hivyo akatoa wito kwa kila mwananchi kushiriki pasipo wasiwasi wowote.

Aliwataka kulinda nchi kwa kuwa babu zao waliiacha ikiwa salama.

Alisema wameanza maandalizi kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa amani na utulivu.

‘Uchaguzi unakuja, lazima tujipange vizuri, tuliahidi tutalinda nchi hii, babu zetu walituachia salama, lazima tukabidhi wajukuu zetu ikiwa salama,” alisema.

Alisema kuzuia ni bora kuliko kuponya na kuwataka askari kuimarisha ulinzi kwenye maduka makubwa na sehemu za mikusanyiko.

Aidha, alitoa wito kwa wazazi na walezi kulea watoto wao kwa uadilifu na kufichua wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles