26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Kaya 22,540 hazina vyoo Mara

Shomari Binda -Musoma

KAYA 22,547 mkoani Mara zimebainika hazitumii vyoo na ziko hatarini kupata magonjwa ya kuambukizi kama kipindupindu.

Akitoa taarifa kwa wajumbe wa timu ya hamasa ya kitaifa ya kampeni ya uhamasishaji ya matumizi bora ya vyoo ijulikanayo kama Usichukulie poa nyumba ni choo, inayoratibiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Ofisa Afya Mkoa wa Mara, Bunija Mhando alisema hali ya matumizi ya vyoo sio nzuri.

Mhando alisema kumekuwa na uhamasishaji mara kwa mara juu umuhimu wa kutumia vyoo, lakini bado wapo wananchi ambao hawajachukua hatua ya kubadilika.

Alisema ofisi yake bado inaendelea kufanya uhamasishaji na kuiomba timu ya kitaifa ya uhamasishaji kuongeza nguvu ili kila mwananchi achukue hatua ya kutumia choo kwenye maeneo yao.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, alisema haikubaliki kuona hadi sasa bado kuna watu hawatumii vyoo.

Aliagiza kila mtendaji kwenye halmashauri zote za mkoa huo kutimiza wajibu wake kuhakikisha anafikisha elimu na kila kaya inakuwa na choo.

“Hii ni aibu, hatuwezi kukubali kuendelea kuwa nayo, nataka baada ya siku 60 kila kaya iwe na choo, baada ya hapo naiomba timu ya hamasa ifike tena mkoani hapa kuangalia utekelezaji wake,” alisema Malima.

Mkuu wa hamasa, msanii Mrisho Mpoto, alisema wananchi wasisubiri wazungu kuja kuwafundisha kutumia vyoo na kunawa mikono kwa kuwa ni suala la aibu.

Alisema gharama za kujenga choo bora na ndoo ya kunawia mikono ni nafuu, hivyo kila mwananchi achukue hatua bila kusubiri kuletewa watu kutoka nje kuwafundisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles