27.6 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

IGP Sirro awakumbusha askari wajibu wao

Na SARAH MOSES -DODOMA


MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, amewataka maofisa wa polisi kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili kwa sababu askari akikosea jambo moja Serikali inaonekana haifai.

Kauli hiyo aliitoa jijini hapa juzi, alipofunga mafunzo ya uongozi kwa maofisa wakuu wa polisi yaliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi.

Alisema kazi ya askari ni kulinda dola na si kuivunja.

“Kesi nyingine zinafeli kwa sababu ya kukosa weledi, hivyo kupitia mafunzo waliyopewa wanatakiwa kuwa tofauti zaidi katika utendaji wa kazi, hata usikilizaji wa kesi nao unahitaji weledi,” alisema.

Pia alisema kamanda wa polisi anategemewa kutenda haki katika mkoa wake na unamtegemea kusimamia sheria zote na kutokuwa na maadili mema, ikiwamo upokeaji wa rushwa, ni vitu ambavyo havitakiwi.

“Kama kuna sehemu ulikuwa unakunywa hadi unalala huko huko acha mara moja, kwa sababu uongozi umetimiza wajibu wake, hivyo makamanda imebaki kazi kwenu na muache kufanya kazi kwa mazoea.

“Kila alipo Mtanzania yupo polisi na usipotimiza wajibu wako utamkwaza raia, hivyo basi itakuwa ni aibu kubwa mkirudi katika maeneo yenu mkiwa hamjabadilika au mkiwa mmeharibikiwa zaidi,” alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Kamishna wa Fedha na Mipango wa Jeshi la Polisi, Leonard Paul, alisema endapo maofisa wa polisi wakifanya kazi kwa weledi na kwa kufuata maadili, watakuwa na ushirikiano mzuri na wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles