25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

IGP Siro amepwa siku saba kushughulikia chakula cha mbwa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amempa IGP Simon Sirro siku saba kushughulikia bajeti ya chakula cha mbwa wawili wanaotumika kulinda ulinzi na usalama.

Simbachawene ametoa agizo hilo leo Ijumaa Januari 8, jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya kikazi alipotembelea maeneo ya Jiji hilo.

Amesema kuwa mbwa hao wawili kati ya saba hawana bajeti ya chakula wanatakiwa kupewa bajeti kwa sababu wanafanya kazi kubwa kuliko binadamu.

“Mbwa hawa ni askari wanaotumika sana ni nimemwagiza IGP ndani ya siku saba ahakikishe Mbwa wote saba wapo kwenye bajeti.

“Katika mbwa saba wapo mbwa watano wenye bajeti na wawili hawapo kwenye bajeti ambapo kwa mwezi wanatumia Sh laki nane, inatakiwa wote wawepo kwenye bajeti,” anasema Simbachawene

Aidha, Simbachawene amempa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa zawadi ya gari kama ishara ya pongezi kwa utendaji wake ikiwa na kudhibiti uhalifu na kupungua kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wake, Mambosasa, ameshukuru kwa zawadi hiyo na kusema ataendelea kupambana na kudhibiti uhalifu.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Chakula cha mbwa mmoja ni zaidi ya shilingi 800,000 kwa mwezi ???? Are we serious?
    Hicho chakula kinatoka Ulaya kwa njia ya ndege? Au kinaungwa kwa dhahabu? Jamani hebu tuwe na busara

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles