Jakarta, Indonesia
Kamati ya usalama wa usafiri nchini Indonesia jana imetangaza kuwa waokoaji wamethibitisha mahali kilipo kisanduku cheusi cha ndege ya abiria ya kampuni ya Sriwijaya Air iliyoanguka baharini.
Jumamosi alasiri, ndege ya abiria aina ya Boeing 737-500 ya kampuni ya Sriwijaya Air iliyokuwa na abiria 62, ilipoteza mawasiliano dakika chache baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Jakarta, na baadaye ikathibitika kuanguka baharini karibu na kisiwa cha Laki.