24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

IGP awapandisha vyeo askari  polisi

Na BENJAMIN MASESE

-MWANZA

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro imewapandisha vyeo askari sita kwa kushiriki matukio mbalimbali ya kukabiliana na majambazi sugu katika Mkoa wa Mwanza.

Askari hao wamepata ofa hiyo baada ya utendaji kazi mzuri huku mmoja akipatiwa cheti cha heshimna na utendaji bora kutokana na  kufaulu vizuri katika mafunzo ya taaluma mbalimbali ndani ya jeshi hilo.

Askari waliotunukiwa vyeo ni pamoja na WP. 12415 Dominika Nnko, G.4745, Rodrick Ndyamukama, G.7087 na Thomas Masingija ambao wamepandishwa kutoka Kostebo kwenda koplo.

Wengine ni F5820 Amon Rubanzibwa na F.8361 Belson Sanga ambao wamepandishwa kutoka koplo kuwa sajenti na kukabidhiwa Sh 400,00 kila mmoja.

Aidha aliyekuwa Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, ASP Levina Jeremia aliyepandishwa cheo na Rais John Magufuli hivi karibuni jijini Dar es Salaam alikabidhiwa cheti cha shukrani na pesa taslimu Sh 800,000 kama sehemu ya kutambua mchango wake katika mafunzo aliyoshiriki ndani na nje ya nchi na kufaulu vizuri.

Akiwatunuku vyeo hivyo jana kwa niaba ya IGP Sirro, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna alisema askari hao wamekuwa mstari wa mbele katika kutimiza wajibu wao na kufanikiwa kuwathibiti na hata kuwaua majambazi sugu waliokuwa na silaha za kivita. 

Kamanda Shanna ambaye hakutaka kuelezea kwa undani kwa kile alichodai kuwa kazi aliyopewa na IGP ni kuwatunukua vyeo na kumwanchia kazi hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John  Mongella.

Mongella aliwashukuru askari  hao kwa uchapakazi wao wa kutimiza wajibu  kwa uadilifu mkubwa na kuleta sifa ndani ya Mkoa wa Mwanza na viongozi wao.

“Kazi yangu leo ni ndogo sana ingawa najua waandishi wana hamu ya kusikia nasemaje lakini nimepewa jukumu na IGP la kuwavisha askari watano vyeo tu, suala la kuzungumza ama kutoa shukrani namwachia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mongella lakini kwa ufupi ni kwamba askari  hao wamefanya kazi kubwa ya kuwadhibiti majambazi wenye silaha nzito tena za kivita, hivyo lazima mchango wao uthaminiwe na kupewa zawadi.

“Leo  mimi nitawavisha vyeo, pia mkuu wa mkoa atawapatia zawadi na kuwakabidhi vyeti vya shukrani, shughuli ya leo imewahusisha vikosi vyote vya jeshi la polisi, magereza, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na majeshi menngineyo,”alisema.

Kwa upande wake, Mongela aliwakabidhi vyeti vya shukrani na zawadi pesa taslimu huku akisema anafurahi kuona anaongoza mkoa ambao ni salama na hauna matukio ya kutisha kutokana na kazi nzuri inayofanywa na jeshi la polisi.

Alisema moja ya idara ambazo zinafanya kazi nzuri bila unyanyasaji na uonevu ni jeshi la polisi na kupongeza kwa  namna wanavyotimiza wajibu wao kwa kuzingatia uadilifu na utawala bora.

“Mmepandishwa vyeo msidhani cheo hicho ni chako peke yako hapana, bali ni mali ya viongozi wote wa mkoa na ndio walioshirikia kutambua mchango wenu hivyo sifa zote ni mkoa na taifa kwa ujumla, binafsi nafarijika kuona tunamaliza mwaka tukiwa salama na bila shaka kesho (leo) tutauanza mwaka mpya tukiwa na furaha na afya njema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles