27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mbunge CCM amtuhumu Waziri kutoa kauli ya kumdharau Waziri Mkuu

Mwandishi Wetu, Dodoma



Mbunge wa Mafia, Mbaraka Dau (CCM), amemtuhumu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaack Kamwele, akidai amekiuka agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, la kupeleka Mafia meli iliyotolewa na mfanyabiashara  Said Salim Bakhressa akidai ni maagizo ya kisiasa.

Dau amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo Jumanne Novemba 6, wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/20.

Alidai kuwa, suala la kupeleka meli hiyo Mafia walilijadili na Waziri Mkuu Majaliwa na akakubali ipelekwe Mafia jambo ambalo hata Profesa Makame Mbarawa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, aliliridhia.

“Sasa hivi nimemfuata na kumkumbusha suala hilo lakini Waziri Kamwele anasema ni kauli za kisiasa, sasa inakuwaje waziri anasema agizo la Waziri Mkuu ni la kisiasa,” alihoji.

Alisema pia alimtuma mbunge mwenzake ili azungumze  na Waziri Kamwele, lakini naye alijibiwa kuwa ili meli ipelekwe huko labda nauli iwe Sh 100,000.

Kabla ya mchangiaji wa mwisho kusimama, Waziri Kamwele alisimama na kusema; “Mbunge wa Mafia amenituhumu kuwa nilitoa maneno yanayoosha nimemdharau Waziri Mkuu, sijawahi kusema hayo maneno na waziri mkuu ila nakumbuka alinipigia simu akanimbia meli hiyo iliyotolewa na mfanyabiashara Bakhresa ifanye safari Mafia, nikatoa maagizo suala hilo liangaliwe kama linawezekana nikaambia meli hiyo inafanyiwa matengenezo,” amesema Kamwelwe akidai kauli ya Dau si nzuri kwa sababu Waziri Mkuu ni bosi wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles