Sakata la Mo laibuka bungeni

0
1839

Mwandishi wetu, Dodoma


Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), ameibua suala la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji kiaina.

Akichangia mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/20, leo Jumanne Novemba 6, Mchungaji Msigwa amesema kwa sasa wawekezaji kutoka nje na wale wa ndani hawama amani.

“Wawekezaji wanajionaje kuwepo katika nchi hii, wapo salama? Takwimu zinaonyesha wawekezaji wa nje wanafunga virago.

“Je wawekezaji wa ndani wakoje? Wana raha? Kama bilionea mkubwa nchi hii anaweza akashikwa, akafichwa, akaachiwa halafu hadi leo hajaruhusiwa kusema alikuwa wapi unadhani nani atakuja kuweka biashara hapa ndani? Haya mambo hatuwezi kufumbia macho, lazima tuyajadili.”

Msigwa amesema kwa sasa kama nchi lazima ijitathimini iko vipi kidplomasia.

“Wenzetu wanatuonaje kama Taifa? Katika historia haijawahi kutokea Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) anaitwa kujieleza,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here