25.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 28, 2024

Contact us: [email protected]

Hotuba ya Rais Kagame aliyowaliza wanachuo Marekani -2

Paul KagameMICHAEL MAURUS NA MITANDAO

WIKI iliyopita, tuliwaletea hotuba ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame aliyoitoa Aprili 25, 2014 wakati kiongozi huyo alipotembelea Chuo Kikuu cha Brandeis kilichopo katika kitongoji cha Waltham, mjini Massachusetts, Marekani na kupata fursa ya kuzungumza na wanafunzi wa chuoni hapo.

Baada ya kuona utangulizi wa hotuba hiyo, hebu endelea kupata uhondo zaidi wa kile alichozungumza Rais huyo juu ya nchi yake ya Rwanda, hii ikiwa ni sehemu ya mwisho ya hotuba hiyo. Endelea…

Kesi zilisikilizwa na kutolewa maamuzi katika ngazi za vijiji. Katika mazungumzo ya kuelezea ukweli kuhusiana na kile walichofanya na kuona, wahusika waliondolewa vifungo au kufanya kazi za kijamii. Kupitia Gacaca, Rwanda ilikuwa imejaribu kutatua kesi milioni mbili ndani ya miaka 10, ikimaliza mchakato huo mwaka 2012.

Ama kwa hakika maridhiano na haki si tukio la kawaida, lakini mchakato wa kitaifa wa muda mrefu ambao unahitaji mazungumzo endelevu katika ngazi zote.

Kwa sasa tunapambana kuona ni vipi tunaanzisha mtazamo mpya juu ya utambulisho wa kitaifa wa Kinyarwanda ambao utatokana na itikadi ya kikabila kama ilivyokuwa katika serikali za awali.

Lengo si kufuta utofauti au kupuuza historia, lakini ni kuwasaidia Wanyarwanda kujiona wenye wajibu mkubwa kwa taifa lao na kujitanguliza mbele katika shughuli zote za ujenzi wa taifa lao.

Wanyarwanda wamekuwa wakisapoti jitihada hizo kwa nguvu zao zote. Ndio maana programu kama Ndi Umunyarwanda au “Mimi ni Mnyarwanda” zimekuwa zikikumbatiwa na watu wetu.

Programu hizo zinatoa mwanga kwa ajili ya majadiliano miongoni mwa raia, zikilenga katika nguvu ya utambulisho wa Mnyarwanda.

Baada ya mwaka 1994, serikali mpya ililazimika kutengeneza upya taifa ambalo lingeweza kutoa huduma ambazo raia wetu wanahitaji na kustahili.

Kutengemaa kumeiwezesha Rwanda kuanza kazi ya kuijenga vyuo vya kidemokrasia na kusaka uhuru na haki za Wanyarwanda, bila mchakato huo, kusingekuwa na maendeleo yoyote.

Ujenzi wa Taifa unahitaji kujipanga upya na katika baadhi ya mambo yaliyoibuliwa mwanzo, tulianzisha sheria mpya na kuwataka mawakala kama Mkaguzi Mkuu, Polisi na mpatanishi ili kuhakikisha uwajibikaji na kudumisha uwezo wa taifa kuweza kujilinda na kurejesha imani kwa wananchi.

Pia tumekuwa tukitumia njia kadhaa za nyumbani kukabiliana na changamoto kadha wa kadha za kijamii na kiuchumi zinazoikabili Rwanda.

Moja ya njia hizo ni pamoja na ile ya Imihigo, iliyokuwa ikitumiwa kabla ya ukoloni ambapo mtu m moja mmoja alikuwa akijiwekea malengo ya kufanikisha mipango yake.

Imihigo kwa Rwanda ya sasa inafanyika kwa mkataba ambapo malengo huwekwa mbele ya jamii na kusainiwa na maofisa wa umma.

Katika mpango huu uliotuwezesha kupata matokeo haya miongoni mwa Wanyarwanda, kwa mfano, matunda mazuri zaidi tuliyoyapata katika kuongezeka kwa huduma ya afya ya mtoto na wajawazito pamoja na wazazi.

Kwa kuendelea, tunaamini kwamba sekta binafsi zitasaidia sana kuhamasisha mabadiliko ya kijamii na kiuchumi.

Tulibinafsisha makampuni yaliyokuwa yakimilikiwa na serikali na kufanya kazi ili Rwanda iwe sehemu ya kuvutia kibiashara na kiuwekezaji.

Matarajio yetu kwa sasa ni kuboresha miundombinu yetu na mtaji kwa wananchi wetu, hivyo tutaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kuchuana katika soko la Dunia na kuifanya Rwanda kuwa nchi yenye kuingiza kipato cha kati hadi mwaka 2020.

Malengo yetu ni kuongeza nafasi kwa kila Mnyarwanda, wakiwamo vijana wadogo wanaotengeneza robo tatu ya idadi ya watu wa Rwanda.

Rwanda inafahamu umuhimu wa jimbo, bara na ushirikiano wa kimataifa. Hii ndio sababu tupo ngangari ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kati, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Madola na Umoja wa Mataifa.

Pia tunathamini uhusiano tunaoufurahia baina yetu na vyuo vikuuu, biashara na mambo mengine makubwa katika nchi yetu.

Wakati suala la kuijenga upya nchi yetu likibaki kwa serikali na watu wa Rwanda, tunaendelea kujifunza. Pia, tupo tayari kujifunza pamoja na wengine: kukubaliana na changamoto; kuwawezesha viongozi kuwajibika; na kuwatanguliza mbele wananchi katika kila jambo tunalofanya.

Tangu mwanzo, Rwanda ililazimika kujaribu na kuwa tayari kuteswa na uamuzi wowote.

Kwa sasa tunafurahia matokeo yaliyopatikana hadi sasa. Kwa sasa tupo tayari hata kuchangia kwasababu pale inapobidi kufanya hivyo ili kuzuia mauaji ya kimbari, tukifanya hivyo kwa kusambaza maelfu ya wapatanishi.

Lakini bado kuna kazi kubwa zaidi mbele yetu na tunajisikia furaha kuona kasi ikiongezeka. Hii ndiyo sababu siku zote tumekuwa tukiwataka wananchi wetu , wanaume kwa wanawake  na vijana wadogo ambao wamewekeza, kuhakikisha kwamba tunakabiliana na changamoto hizi.

Ahsanteni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles