23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Hospitali ya Benjamini Mkapa kujenga kituo cha upandikizaji figo

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

HOSPITALI ya Benjamini Mkapa (BMH) inajenga kituo cha upandikizaji wa Figo (Kidney Transplant Complex) chenye vyumba vya upasuajia kwa anayechangia figo na anayepokea.

Hayo yameelezwa leo Jumanne, Agosti mosi,2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dk. Alfonce Chandika wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya BMH na mwelekeo wake kwa mwaka wa fedha 2023-2024.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wanaondokana na mwingiliano wa mgonjwa anayepandikizwa figo na wagonjwa wengine.

“Tunamwondolea usumbufu kufuata huduma sehemu mbalimbali na kupunguza muda wa kusubili huduma. Kwa kuwa mgonjwa atahudumiwa sehemu moja na vile vile watoa huduma watapunguziwa usumbufu wa kutafuta kufuata vifaa kwenye idara nyingine,” amesema Dk. Chandika.

Amesema wamekuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika kupata matibabu na imepelekea kuwa na vyumba vya upasuaji vichache.

Amesema kwa mwaka huu wanatarajia kuongeza vyumba vya upasuaji ili kukidhi hitaji la wagonjwa.

Pia wanajenga Maabara ya kuchukulia sampuli za wagonjwa, chumba cha wagonjwa mahututi, Famasia (duka la dawa), vyumba vya madaktari.

Amesema huduma za matibabu ya moyo, katika huduma hizi za moyo zimeendelea kuimarika kutoka mwaka hadi mwaka.

Amesema mwaka uliopita wamefanya uchunguzi wa mishipa ya moyo kwa wagonjwa 320, upandikizaji betri wagonjwa 13, watoto waliozibwa matundu kwenye moyo 14, kuweka vizibua njia ya Mishipa ya Moyo (Stents) 54.

Pia huduma ya vipandikizi kwenye magoti na nyonga (Hip and total Knee Replacement) jumla ya wanufaika 72 wamenufaika na huduma hiyo.

Amesema Serikali imetumia Sh milioni 864 ambapo kama wangeenda kupata huduma hiyo nje ya nchi ingeigharimu Serikali zaidi ya Sh bilioni 2.5 ambapo amedai Serikali imeokoa zaidi ya Sh bilioni 1.6.

Aidha katika matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi huduma ya Ubongo na Mishipa ya Fahamu wananchi wamenufaika na huduma hiyo kwa upasuaji wa ubongo 276 na upasuaji uti wa mgongo 237

Dk Chandika amesema pia wameweza kupandikiza uloto (Borne Marrow Tansplant) ambayo imeafanikiwa kwa manufaa makubwa kwa watoto wa nne wamepatiwa matibabu hayo na sasa wamepona.

“Huduma hii inapatikana Tanzania pekee katika ukanda wa Afrika mashariki na Kati na ni Hospitali ya Benjamin Mkapa pekee inayotoa matibabu, gharama za matibabu ni Sh milioni 50 wakati matibabu haya nje ya nchi yanapatikana kwa Sh milioni 120 hadi 135.

“Ni kusema Serikali imedhamiria kuokoa pesa na kuimarisha huduma za matibabu Tanzania,”amesema Dk. Chandika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles