24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Homa ‘Dar Boxing Deby’ yazidi kupanda

Na WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital

MABONDIA wanaotarajiwa kupanda ulingoni katika pambano la ‘Dar Deby Boxing’ lililopewa jina la Mwana Ukome, wamezidi kupigana mkwara kila mmoja akitamba kumchakaza mpinzani wake.

Pambano hilo litafanyika Jumamosi Oktoba 30,2021 kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam likihusisha mambondia mbalimbali.

Bondia Iddi Piarali ambaye anatapanda ulingoni kuzichapa na Ramadhani Shauri, amesema atahakikisha anampiga mpinzani wake kwa K.O.

“Nimejiandaa vya kutosha, mazoezi nimeanza kufanya muda mrefu, nataka kumaliza mchezo mapema siku hiyo kwa kumpika KO,” amesema Piarali.

Naye Selemani Kidunda ambaye amekuwa na rekodi nzuri hapa nyumbani, amesema yeye ni bondia mzoefu na hakuna cha kuhofia kwa mpinzani wake Jacob Maganga, kwani kocha wake wamemuandaa vizuri kila kitu kitaonekana ulingoni.

“Ni kitu kizuri kushirikiana na kocha wako kwa sababu ndiyo anajua ananitengeneza kitu gani. Watu wafike tu siku hiyo ya tarehe 30 wajionee udambwi udambwi, nataka nimfanye kitu ili akikaa ajue mimi mtu mbaya,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles