24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

HIDAYA WA PEPE KALLE: LAZIMA MWANANGU AZIKWE NCHINI


Na Mwandishi wetu    | 

Mama Hidaya Mtumwa maarufu Hidaya wa Pepe Kalle aliyefiwa na mtoto wake Leyla aliyeuawa na mumewe nchini Uingereza amesema mwanawe lazima aje kuzikwa Tanzania.

Aidha amesisitiza kuwa Mjukuu wake Taiyris ambaye ni mtoto wa marehemu aje kuona mahali atakapozikwa mama yake.

Mama Hidaya ameyasema hayo leo mchana nyumbani kwake Kaloleni jijini Arusha ambako ndiko kwenye msiba, alipokuwa akizungumza na Mtanzania Digital.

Aidha, amesema hadi sasa taarifa za awali alizokuwa nazo ni za mwili wa mtoto wake kufanyiwa uchunguzi (postmortem) leo huko Uingereza.

Leyla amefariki usiku wa kuamkia leo baada ya kudaiwa kuuawa na mumewe kwa kuchomwa kisu kwa madai ya kuchelewa kurudi nyumbani usiku sana akitokea disko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles