22.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

HESLB yaanzisha madawati ya malalamiko

Omega NgoleESTHER MNYIKA NA GRACE SHITUNDU, DAR ES SALAAM

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa  utaratibu wa kushughulikia  malalamiko ya wanafunzi wanaopata mikopo katika taasisi za elimu ya juu nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Omega Ngole, alisema kwa sasa wameandaa utaratibu wa kushughulikia malalamiko ya wanafunzi wa elimu ya juu.

“Utaratibu huu ulioboreshwa ni msisitizo na maelekezo ya Serikali ya Agosti 2011 kupitia iliyokuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambayo ilielekeza taasisi zote za elimu ya juu zinazopata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo kuanzisha madawati ya mikopo ili kuongeza ufanisi katika utoaji mikopo,” alisema.

Alisema dawati hilo linatakiwa kusimamiwa na mtumishi teule wa chuo husika mwenye sifa na uhusiano mzuri na jamii na linapaswa kuwa chini ya makamu mkuu wa chuo husika anayeshughulikia taaluma.

Ngole alisema kwa sasa vyuo vyote vina maofisa mikopo ambao wanawajibika kutafuta suluhisho la suala linalowasilishwa na kulitolea majibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles