28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

HECHE AITAKA SERIKALI KUTOKUWATUMIA POLISI KISIASA

Na FREDRICK KATULANDA

MWENYEKITI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Serengeti, John Heche, ameitaka serikali kutotumia polisi  kuzuia mikutano halali ya vyama vya upinzani.

Akizungumza   Mwanza juzi,  Heche alisema  wakati Chadema  kinakumbana na upinzani wa kufanya mikutano yake   mpaka   ya ndani,   wenzao CCM wamekuwa wakifanya mikutano kila siku bila ya kubughudhiwa na polisi.

Heche alisema hali hiyo inaonyesha  Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikiwazuia wapinzani na wenzao wakiendelea na siasa.

“Mikutano yetu inazuiwa wakati ipo kwa mujibu wa katiba, lakini CCM  inafanya kampeni za uchaguzi wa mwaka 2020.

“Hatutanyamaza tutaendelea kupigania haki hii na ndiyo maana chama chetu kimefungua kesi mahakamani,” alisema.

Agosti 4, mwaka huu, Heche alikamatwa na polisi akituhumiwa kuchochea wananchi kuvamia Mgodi wa Dhahabu wa North Mara ambao ni Mali ya Kampuni ya Dhahabu ya Acacia.

Pamoja na kuhamasisha kilimo cha bangi, alisema kwa sasa viongozi wa Chadema wamekuwa wakikamatwa na kubambikiwa kesi zisizo na kichwa wala miguu.

Alisema CCM, polisi na Serikali wasidhani kuwa kukaa kwao kimya ni kuogopa kuwekwa ndani bali wameamua kukutana katika vikao vya ndani kujadiliana namna ya kukabiliana nao na kujifananisha na moto wa pumba ambao huwaka chini kwa chini.

Alisema iwapo wanadhani Chadema imetulia kwa sababu ya kuogopa kukamatwa au kesi watakuwa wamejidanganya na kusisitiza kuwa wapo na punde watauona moto wao.

“Katika kanda yangu ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara, wapo viongozi ambao walikamatwa na kufungwa lakini tumekata rufaa na wapo nje.

“Mimi mwenyewe   na Mbunge Ester Matiko pia tulikamatwa kwa kesi ambazo ukiziangalia unajua zina malengo ya siasa.

“Sasa katika kikao hiki tumekubaliana kuwalinda viongozi wetu na kuwalinda wanachama wote watakaokamatwa kwa malengo ya siasa na kuwapa msaada wa sheria au msaada wowote utakaohitajika,”alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles