27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI MKUU AONYA AJIRA ZA WATOTO MASHAMBANI

Na Mwandishi Wetu

-TABORA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amewataka wakazi wa Mkoa wa Tabora kuwapeleka watoto wao shule na waache kuwatumia kama vibarua kwenye mashamba ya tumbaku.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo juzi wakati akizungumza na watumishi wa idara za kilimo na ushirika na viongozi wa wilaya ya mkoa huo katika kikao alichokiitisha ili awape maagizo maalumu.

“Ninasisitiza kuanzia sasa jamii iwapeleke watoto shule kuanzia elimu ya awali hadi sekondari na tuache kuwatumia watoto wadogo kama vibarua kwenye mashamba ya tumbaku. Wakuu wa wilaya simamieni eneo hili la kuondoa watoto kwenye ajira,” alisema.

Katika hatua nyingine, Majaliwa alitumia fursa hiyo kusisitiza viongozi wa mkoa huo wasimamie elimu ya mtoto wa kike na kuhakikisha kuwa wanahitimu elimu ya sekondari.

“Kuna tatizo la mimba kwa watoto wa shule. Eneo hili pia linahitaji usimamizi ili kuwalinda watoto wa kike wamalize elimu yao. Tuwalinde wanaposoma elimu ya msingi na sekondari, wakishafika vyuo vikuu watakuwa wamepevuka na kuweza kufanya maamuzi ya kujilinda,” alisema.

Akihutubia kwenye mikutano ya hadhara wakati wa ziara yake ya siku nne mkoani Tabora, Waziri Mkuu aliwaasa vijana wa kiume wasithubutu kuoa wanafunzi kwani kwa kufanya hivyo, wataishia kufungwa jela miaka 30.

Pia aliwaasa wazazi wanaoamua kuwaoza mabinti zao ili wapate mahari, nao pia wanakabiliwa na hatari hiyo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles