23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Hatima rufaa ya Zombe kujulikana leo

 Abdallah Zombe
Abdallah Zombe

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Rufaa leo inatarajia kutoa hukumu dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, ACP Abdallah Zombe na  wenzake.

Hukumu hiyo ya mahakama itatolewa na jopo la majaji watatu, Benard Luanda, Sauda Mjasiri na Semistocles Kaijage baada ya kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kuwaachia huru maofisa hao.

DPP anapinga wajibu rufani hao kuachiwa katika kesi ya mauaji ya kukusudia ya wafanyabiashara watatu wa madini wa Mahenge mkoani Morogoro na dereva teksi wa Manzese  Dar es Salaam.

Wajibu rufani wanadaiwa kutenda makosa hayo Januari 14, 2006, katika Msitu wa Pande uliopo Mbezi Luis, jijini Dar es Salaam.

Wafanyabiashara waliouwawa ni Sabinus Chigumbi  au Jongo na ndugu yake Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe pamoja na dereva teksi Juma Ndugu.

Mbali na Zombe, washtakiwa wengine walikuwa ni ASP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle na Koplo Rajabu Bakari.

Septemba 17, 2009, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam  iliwaachia huru washtakiwa wote ikisema kuwa baada ya kusikiliza ushahidi na hoja za mawakili wa pande zote imeridhika kuwa washtakiwa hawakuwa na hatia ya mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Jaji Salum Massati aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo alisema kuwa amebaini kuwa walioshtakiwa si walioua, bali wauaji hawakuwepo mahakamani.

Mahakama iliagiza Jamhuri kuwasaka na kuwafikisha mahakamani wauaji halisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles