20.8 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Tetemeko likitokea ingia uvungu wa kitanda – Mtaalamu

_91169090_10

NA HADIA KHAMIS, DAR ES SALAAM

WATAALAMU wa masuala ya miamba wamewatahadharisha wananchi kujiandaa kisaikolojia kuhusu tetemeko dogo la ardhi linalotarajia kutokea.

Tahadhari hiyo imetolewa ikiwa ni siku sita tangu kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi mkoani Kagera lililosababisha vifo vya watu 17.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Jiografia ya Mazingira, Philip Mwanukuzi, alisema ipo haja kwa Serikali kutoa elimu ya kutosha kwa wakazi wanaoishi katika maeneo yanayokumbwa na matetemeko ili kila mkazi aelewe chakufanya.

Alisema kama tetemeko litakukuta ukiwa ndani ya nyumba unashauriwa kukaa chini ya uvungu wa kitanda au meza, ama kusimama kwenye makutano ya kuta, kukaa mbali na madirisha na makabati ya vitabu.

Mwanukuzi alisema ni vyema kwa waathirika wa tetemeko la ardhi kutojenga katika sehemu wanazoishi kwa sasa hadi hapo watakapopatiwa ushauri na wataalamu.

Akitoa taarifa kuhusu tetemeko la ardhi, Kaimu Mkuu wa Idara ya Idrolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Elisante Mshiru, alisema ni suala la kawaida na hutokea kila mwaka duniani kote.

Alisema tetemeko lililotokea mkoani Kagera ni la nne kutokea kwa kipindi cha miezi 10 iliyopita nchini.

“Matetemeko ya ardhi yanapishana, kipimo cha juu kabisa ni magritude 10, matetemeko hayo makubwa ndiyo yanayosababisha vifo na hutokea mara 150 hadi 1,500 kwa mwaka ingawa hutofautiana na sehemu yanayotokea,” alisema Mshiru.

Alisema tetemeko lililotokea mkoani Kagera lina ukubwa wa kipimo cha skeli ya richter 5.9 ambalo kitaalamu huitwa ‘mainshock’ (tetemeko kuu).

Mshiru alisema tetemeko linalotarajiwa kutokea linaweza kuwa na ukubwa wa skeli ya richter 4.4 au 4.5.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles