22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Hassan Ndonga, Oscar Richard wataka kuzichapa juani

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

ZIKIWA zimebaki saa chache kabla ya kupanda ulingoni katika pambano lao la Safari ya Beach, mabondia Hassan Ndonga na Oscar Richard, nusura wazichape wakati wa kupima uzito jana Oktoba 21,2023 kwenye viwanja vya Faru Mpakani Mabibo, jijini Dar es Saalam.

Mapambano ya Safari ya Beach yatahusisha mabondia zaidi ya 30 yatakayofanyika leo Oktoba 22, 2023 kwenye fukwe za Rongoni, Kigamboni, jijini lakini Ndonga na Oscar ndiyo wenye pambano kubwa.

Bondia Oscar Richard akitunisha misuli baada ya kupima uzito.

Mabondia hao wenye upinzani mkubwa na mashabiki wengi waliingia uwanjani hapo kila mmoja akiwa na idadi kubwa ya mashabiki ambao walitambiana ubora wa watu hao kwa kutupiana vijembe.

Licha kuwa na jua kali mashabiki hao hawakujali chochote, kila mmoja alitaka kuhakikisha anazima ngebe za mpinzani wake kwa kupigana mikwara ambayo iliwapandisha mzuka Ndonga na Oscar na kutaka kuzichapa wakati wakutunishiana misuli.

Wakizungumza baada ya kupima uzito, mabondia hao ambao ni majirani wanaofanya mazoezi kambi tofauti, wamesema kwa kesho wanaweka ujirani pembeni, huku kila mmoja akiahidi kuibuka kidedea.

Mashabiki waliojitokeza katika viwanja vya Faru Mpakani, Mabibo, Dar es Salaam kushuhudia shughuli ya kupima uzito kwa mabondia Hassan Ndonga na Oscar Richard.

“Kikubwa ninachowaahidi mashabiki waje washuhudie burudani, hii ni derby, ninajua huyu ni bondia mzuri lakini kwangu bado na hataweza kumaliza raundi tatu,” ametamba Oscar ambaye anatoka kambi ya Naccoz Gym.

“Mimi ndiyo Tyson wa Bongo hakuna wakunisumbua mwenye uzito wangu, mashabiki walimzoea Hassani Ndonga sio yule, nakuja na staili nyingine. Hii ndiyo mara ya kwanza tunakutana, sisi ni majirani tutajuana,” amesema Ndonga timu Makatuni Pesa.

Akizungumzia maandalizi Mratibu wa Matukio wa Peaktime Media waandaji wa mapambano hayo, Bakari Khatibu, amesema kila kitu kipo tayari mabondia wote wapo katika hali nzuri, huku akitaja kiingilio kuwa ni sh. 5000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles