22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Hashimu Rungwe ahojiwa kwa saa mbili polisi

Na ASHA BANI

-DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma), Hashimu Rungwe, amehojiwa kwa saa mbili na Jeshi la Polisi Dar es Salaam na kuachiwa.

Rungwe jana alifika katika Kituo cha Polisi Oysterbay saa nne asubuhi.

Alipata wito wa kuitwa polisi juzi baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari uliokutanisha vyama nane vya upinzani.

Akizungumza na Mtanzania nje ya kituo cha polisi jana, Rungwe alisema alitumia saa mbili kwenye mahojiano yaliyoanza saa nne asubuhi na kumalizika saa sita mchana.

“Nimeitikia wito, lakini nimeulizwa nilichozungumza na nikaandika maelezo yangu, kikubwa waliuliza kwanini nilifanya mkutano wakati kuna rufaa mahakamani.

“Katika maelezo yangu nikasema ni kwa sababu kuna uchaguzi wa madiwani na nikaeleza mengine, wakaniambia basi ondoka na ndio hivi natoka, hakuna masharti mengine waliyonipa,” alisema Rungwe.

Juzi Rungwe alifanya mkutano na waandishi wa habari ambao vyama vya ACT-Wazalendo, CCK, Chadema, DP, NCCR-Mageuzi, NLD na UPDP pia vilishiriki.

Katika mkutano huo, vyama hivyo vilitangaza msimamo wa kutoshiriki uchaguzi mdogo katika kata 32 unaotarajiwa kufanyika Juni 15.

Sababu walizotoa ni kutokana na  kusimamiwa na wakurugenzi kinyume na uamuzi wa Mahakama Kuu.

Mkurugenzi wa Uchaguzi (NEC), Athuman Kilamia, alisema hawajavunja sheria yoyote na wala hawajaingilia hukumu ya mahakama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles