26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

HARIRI AREJEA LEBANON

BEIRUT, LEBANON


WAZIRI Mkuu wa zamani wa Lebanon, Saad al-Hariri amerejea hapa juzi jioni, ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipotangaza kujiuzulu wadhifa huo akiwa Saudi Arabia, zaidi ya wiki mbili zilizopita.

Kujiuzulu kwake ambako kulitangazwa kupitia kituo cha televisheni nchini humo, akionekana dhahiri kutokuwa katika hali ya kawaida, kulisababisha mzozo wa kimataifa wa kisiasa.

Hariri alitangaza kujiuzulu akisema usalama wake uko shakani iwapo atarudi Lebanon, akililenga kundi la wanamgambo wa Hezbollah linaloungwa mkono na Iran.

Iran ikaituhumu Saudi Arabia kuwa nyuma ya njama hizo za kuichafua na kundi hilo, kabla ya mzozo huo kuzifanya Marekani na Ufaransa, ambazo ni mshirika wa Hariri katika eneo la Mashariki ya Kati kuingilia kati.

Kabla ya kujiuzulu, Hariri aliongoza Serikali ya mseto, iliyolishirikisha pia kundi la Hezbollah ambalo ni hasimu wake.

Kupitia juhudi za Ufaransa, Hariri aliondoka mjini Riyadh mwishoni mwa juma lililopita.

Kabla ya kuwasili Beirut, Hariri alitua kwanza nchini Cyprus ambako alizungumza na Rais wa kisiwa hicho, Nicos Anastasiades.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles