24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

DK. SHIKA AONYWA KUVURUGA MNADA WA NYUMBA ZA LUGUMI KESHO

 

Mnada wa kuuza nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi, unatarajiwa kurudiwa kesho safari hii ukiwa na masharti magumu zaidi baada ya ule wa awali kuvurugwa na Dk. Louis shika.

Katika mnada huo, uliofanyika Novemba 9, mwaka huu Dk. Shika alishinda mnada alinunua nyumba hizo lakini akashindwa kulipa asilimia 25 ya fedha kama masharti ya mnada yanavyotaka.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono, Scholastika Kevela, amesema walikaa pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuweka masharti magumu ili kuepuka kuvurugwa kwa mnada wa kesho.

Kevela amesema kama Dk. Shika anaamini mabilioni yake kutoka Urusi yameingia atekeleze masharti ya mnada lakini kama anafikiria kufanya tena mzaha hawatampokea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles