28.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

MASAUNI APEWA MALALAMIKO YA WAVUVI

Na SHOMARI BINDA-RORYA


WAVUVI wa mkoani Mara, wametoa malalamiko yao kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaun, juu ya kuvamiwa na kuporwa mali zao.

Mali zinazodaiwa kuporwa ni mashine za boti, fedha na mafuta  kutoka kwa wahalifu wa nchi jirani wakiwa na silaha za moto.

Wakizungumza baada ya kutembelewa na Waziri Masaun katika eneo la ukusanyaji wa samaki la Busurwa wilayani Rorya, baadhi   walisema wanaumia na kunyanyasika wakiwa ndani ya nchi yao.

Akitoa kilio cha wavuvi, Richard Masero alisema kutokana na ziara  hiyo kwa mara ya kwanza wameona kuwapo doria za polisi ziwani na kuomba ziwe endelevu.

Akijibu malalamiko yao, Waziri Masaun alisema Serikali ipo kwenye maandalizi makubwa ya kufanya ulinzi wa kutosha ili wafanye wavuvi kufanya shughuli zake kwa amani.

Alisema katika kufikia lengo la kulinda usalama wa wavuvi na mali zao katika kudhibiti ulinzi, kikosi cha ulinzi wa ziwani (Polisi Marine) kimeanza kuimarishwa ili kiweze kufanya kazi na kuhakikisha usalama ziwani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles