25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

VIONGOZI URUSI, MISRI WAJADILIANA KUHUSU SYRIA

MOSCOW, URUSI


RAIS wa Urusi, Vladimir Putin, amemtaarifu mwenzake wa Misri, Abdel Fattah el-Sisi kuhusu maendeleo ya mipango yake mipya nchini Syria, ambako oparesheni zake za kijeshi dhidi ya magaidi zimekamilika.

Taarifa iliyotolewa jana na Ikulu mjini hapa, ilieleza kuwa viongozi hao wawili walijadiliana juzi kwa simu na Rais Putin alimwelezea mwenzake jinsi hali ilivyo kwa sasa katika maeneo hayo.

“Pande zote mbili zilikubaliana umuhimu wa kuwapo kwa Baraza Kuu la Taifa la Syria na kuwapo kwa wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ya raia wa nchi hiyo kama inayoonyeshwa katika mpango wa sasa wa Urusi,” ilieleza taarifa hiyo ya Kremlin kwa vyombo vya habari.

Mbali na hilo, taarifa hiyo ilieleza kuwa viongozi hao walizungumzia umuhimu wa kuunganisha jitihada za pamoja katika kuunga mkono jitihada za kisiasa, kidiplomasia na kibinadamu za hapa Urusi kama ilivyokubaliwa katika makubaliano ya Astana.

“Katika majadiliano hayo, viongozi hao wawili walijadiliana kuhusu mazungumzo ya hivi karibuni kati ya Putin na Rais mwenzake wa Syria, Bashar Assad na masuala yaliyojiri katika mkutano wa karibuni uliohusisha mataifa ya Urusi, Iran na Uturuki,” ilifafanua taarifa hiyo.

Iliongeza kuwa Putin na El-Sisi pia walijadiliana masuala ya ushirikiano katika miradi mbalimbali, ukiwamo wa uzalishaji wa nyuklia na huku wawili hao wakionyesha kuridhishwa na ushirikiano uliopo kwa sasa baina ya mataifa hayo mawili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles