22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

HAPATOSHI LIGI KUU ENGLAND LEO

LONDON, ENGLAND

KOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, leo atakuwa na kibarua kizito kwenye Uwanja wa Emirates wakati kikosi chake kikiwa kinawakaribisha wapinzani wao wa jijini London, Tottenham.

Wenger bado hana furaha sana na kibarua chake ndani ya kikosi hicho japokuwa mmiliki wa klabu hiyo, Stan Kroenke, ambaye anamiliki asilimia 67.05 za hisa, kumpa matumaini ya uwepo wake.

Mashabiki wa Arsenal bado hawana imani na kocha huyo, wanatamani aondoke muda wowote hasa pale matokeo yanapokuwa mabaya kwa upande wao.

Leo kocha huyo anajaribu kutaka kuwaaminisha kuwa yeye bado ana nafasi ya kuwa kocha ndani ya kikosi hicho kwa kuwafunga wapinzani hao. Wenger atakuwa na wakati mgumu sana endapo atapoteza mchezo huo kwa kuwa mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu alikubali kichapo cha mabao 3-1 kwenye uwanja wa Etihad dhidi ya Man City ambayo inaonekana kuwa bora msimu huu.

Kwa upande wa Tottenham, wanaonekana kuwa bora msimu huu dhidi ya Arsenal, kabla ya mchezo wa leo Tottenham wanashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi 23 sawa na Man United wanaoshika nafasi ya pili wakitofautiana kwa idadi ya mabao. Wakati huo Arsenal ikishika nafasi ya sita ikiwa na pointi 19.

Nafasi ya ushindi kwa Arsenal inaonekana kuwa ndogo, lakini wanabebwa na kuwa kwenye uwanja wa nyumbani, lakini safu ya ushambuliaji ya Tottenham ambayo inaongozwa na Harry Kane imekuwa ikifanya vizuri siku za hivi karibuni.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa Aprili 30, mwaka huu huku Tottenham wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani na kufanikiwa kushinda mabao 2-0, lakini leo Tottenham wapo ugenini je, wataweza kuendeleza ubabe wao? Chochote kinaweza kutokea.

Michezo mingine ambayo itapigwa leo ni pamoja na Manchester United wakipambana na Newcastle, huku Chelsea wakisafiri na kuwafuata West Brom, Liverpool wao watawakaribisha Southampton, wakati huo Leicester City wakiwakaribisha vinara wa ligi hiyo, Manchester City.

Crystal Palace watakuwa nyumbani na kuwakaribisha wapinzani wao Everton, huku Burnley wakipambana na Swansea City na Bournemouth wakiwakaribisha Huddersfield Town.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles