29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

SERENA WILLIAMS AFUNGA NDOA

LOUISIANA, NEW ORLEANS

BINGWA namba moja kwa ubora wa mchezo wa tenisi duniani kwa upande wa wanawake, Serena Williams, amefanikiwa kufunga ndoa na baba wa mtoto wake, Alexis Ohanian.

Nyota huyo wa tenisi mwenye umri wa miaka 36 na milionea Ohanian mwenye umri wa miaka 34 ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Reddit, waliamua kuwakutanisha mastaa mbalimbali duniani kwenye Ukumbi wa Contemporary Arts Centre, uliopo New Orleans.

Baadhi ya mastaa ambao walipewa mwaliko wa harusi hiyo ni pamoja na Beyonce na mama yake, Tina Knowles, Kim Kardashian, Kelly Rowland, Selita Ebanks, Anna Wintour ambaye ni mhariri wa jarida la Vogue pamoja na Colton Haynes.

Wengine ni Eva Longoria, Jose Baston, Caroline Wozniacki ambaye ni nyota wa tenisi nchini Denmark, nyota wa kikapu, David Lee na wengine wengi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye mtandao wa Daily Mail, harusi hiyo imekadiriwa kutumia zaidi ya dola milioni 1, ambazo ni zaidi ya bilioni mbili kama ilivyo kwenye ndoto za wawili hao.

Harusi hiyo ikiwa inaendelea, kocha wa zamani wa Serena, Patrick Mouratoglou, alitumia ukurasa wake wa Instagram kumtakia kila la heri staa huyo. “Kwa hisia kali nimeamua kukutumia ujumbe huu kwa kukutakia kila la heri katika maisha yako mapya ya ndoa, ikiwa hii ni siku yako muhimu sana, nakuombea ndoa yako iwe na furaha kila wakati na mume wako Alexis Ohanian.” Aliandika.

Kupitia ukurasa wa Twitter, Serena aliandika: “Hii ni siku yangu ya furaha kubwa, najiona kuwa mtu wa pekee kwa kufanikisha harusi, naweza kusema kuwa ndoto yangu sasa imekamilika, nawashukuru wote walioungana na mimi katika siku hii muhimu katika maisha yangu,” aliandika Serena.

Ndoa hiyo imefungwa ikiwa ni miezi miwili tangu wawili hao wafanikiwe kupata mtoto wao wa kwanza ambaye wamefanikiwa kumpa jina la Alexis.

Wawili hao walianza kuwa kwenye uhusiano tangu walipokutana kwa mara ya kwanza Oktoba 2015, lakini hawakutaka kuweka wazi uhusiano huo, lakini Desemba mwaka jana waliamua kuanika baada ya Alexis kumvisha pete staa huyo wa mchezo wa tenisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles