26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

KIONGOZI WA KUNDI MAFIA AFIA JELA

ROMA, ITALIA

MWANACHAMA sugu wa kikundi cha Mafia maarufu kama ‘bosi wa mabosi’ Salvatore “Toto” Riina, amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa kansa akiwa gerezani. Riina amefariki akiwa na umri wa miaka 87 ambapo alikuwa akitumikia kifungo cha maisha jela na inaaminika kuwa alikuwa ametoa amri ya kuuawa watu 150.

Mkuu huyo aliyekuwa akiogopwa sana alitumia karibu robo karne akikimbia mkono wa dola kabla ya kukamatwa mwaka 1993. Inaaminika alifanikisha mauaji mengi zaidi akiwa jela. Pamoja na kansa ya ini, Toto aliaminika pia kuugua ugonjwa wa moyo na ule wa kutetemeka yaani Parkinson.

Riina amekuwa katika hali ya kuwa nusu kaputi na familia yake ilikuwa imepewa ruhusa maalumu ya kumtembelea gerezani katika hospitali maalumu mjini Parma, ulioko Kaskazini mwa Italia.

Riina alizaliwa mwaka 1930  na wakulima masikini huko  Corleone, Sicily – ambako pia ndio mahala alipozaliwa Don Corleone, ambaye alicheza kama baba wa ubatizo katika filamu ya Francis Ford Coppola.

Baba yake aliuawa akiwa na miaka 13 na akiwa na miaka 19 alikuwa tayari amejiunga na kikundi cha     Mafia kilichoko mji aliokulia, ambako ndipo alipofanya mauaji yake ya kwanza.

Riina alichukua udhibiti wa kundi la Cosa Nostra Crime katika miaka ya 1970. Sifa yake ya ukatili ilifanya watu wamwite  kwa jina la utani la “The Beast.” Alitumia miaka 24 akiwa mafichoni katika Kisiwa cha Sicily.

Mwaka 1992, majaji wawili ambao walikuwa hawalitaki kundi la Mafia, Giovanni Falcone na Paolo Borsellino,  waliuawa katika kile kilichoitwa kama ni vita ya Riina’ dhidi ya dola. Mwaka mmoja baadaye alikamatwa.

Akiwa amewekwa ndani, Riina alitoa maagizo kwa kikundi chake cha Mafia kumuua kijana wa miaka 13 ambaye alikuwa ametekwa ili kumzuia baba yake asitoe siri za Mafia. Kijana yule alinyongwa na mwili wake uliyeyushwa kwa asidi.

Riina alifungwa chini ya kifungu cha 41 cha sheria ya magereza inayoagiza kutolewa kwa ulinzi mkali kwa Mafiosos ikilenga kuhakikisha kuwa wafungwa sugu hawapati nafasi ya kuwasiliana na wenzao walioko nje.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Riina alisikika akisema kuwa hajutii chochote. “Hawawezi kunivunja mimi hata kama wakinifunga kwa miaka 3,000,” ilieleza ripoti ya Shirika la habari la AFP. Mtoto wa kwanza wa jambazi huyo, Giovanni, anatumikia kifungo cha maisha jela kwa makosa ya mauaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles