26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Halotel yamzawadia Gari jipya aina ya Mazda CX5 mshindi wa kampeni ya Kivumbi na Halotel

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya simu ya Halotel leo imetoa na kukabidhi zawadi kubwa ya gari aina ya Mazda CX5 kwa mshindi wa kampeni hii iliyokwenda kwa jina la “Kivumbi na Halotel” Kampeni hiyo ilizindulia kwa lengo la kutoa zawadi kwa watumiaji wa mtandao wa Halotel ikiwa ni muendelezo wa kusheherekea miaka 8 ya utoaji huduma za mawasiliano nchini.

Kampeni ya Kivumbi na Halotel ilidumu kwa muda wa miezi mitatu (03) kuanzia mwezi oktoba 2023 ikiwa na lengo la kutoa zawadi kwa watumiaji wa mtandano wa Halotel kama sehemu ya kurudisha shukurani kwa wateja wake.

Kipindi cha Kampeni kulikuwa na zawadi za na washindi wa wiki walijishindia zawadi mbalimbali kama Simu aina ya Samsung A14 yenye uwezo wa teknolojia ya 5G pia ina uwezo wa 128GB, pamoja na laini ya Halotel na 10GB.

Samsung A34 yenye uwezo wa teknolojia ya 5G pia ina uwezo wa 128GB pamoja na laini ya Halotel na 5GB. Router yenye laini ya Halotel na 5GB. Pia washindi 165 wa kila wiki walijishindia vocha za 5,000 kila mmoja.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo la kukabidhi gari kwa mshindi katika duka la Halotel lililopo Pam Village Mikocheni mkuu wa kitengo cha Biashara Halotel, Abdallah Salum alisema kuwa katika kuhakikisha tunajali na kuthamini wateja wetu ikiwa ni muendelezo wetu wa sherehe za kusheherekea miaka nane ya Halotel toka kuanzishwa kwake hapa nchini na kutoa huduma ya mawasiliano kwa watanzania, tumeona ni vema kutoa zawadi mbalimbali kwa wateja ili tufurahi nao pamoja, maana wao wanamchango mkubwa katika kukua kwa mtandao wetu, hivo sisi kama Halotel tunalitambua hilo na tunalithamini sana.

Na leo hii tunathibitisha hilo kwa kukabidhi zawadi hii ya gari kwa mshindi wa kampeni yetu ya Kivumbi na Halotel.

“Tutaendela kutoa huduma bora kwa gharama nafuu ili kuwezesha urahisi wa upatikanaji wa huduma za mawasiliano nchini. Ili kila Mtanzania atumie Halotel kwasababu kuna furaha. Aliongezea kusema hayo Salum.

Akiongea baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya gari Mazda CX5 mshindi ambaye ni Kassim Seif Mbufu alisema, “Najisikia furaha na nimefarijika sana kushinda gari, mimi ni mstaafu hivo kushinda gari hii nimefurahi sanaa nawaomba Watazanzania wezangu tuendelee kutumia mtandao wa Halotel kwasababu huduma zao ni nzuri na nafuu pia mambo mengine mazuri kama haya utayapata ukiwa na Halotel”.

Kampuni ya simu ya Halotel inaendelea kuwahakikishia wateja wake kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu hasa katika kuendelea kusambaza huduma za mawasiliano nchi nzima. Hii ni katika kuonesha jinsi inavyothamini na kujali jamii ya watanzania kwa nyanja mbalimbali, za kijamii, mawasiliano bora yanaleta tija katika sekta zingine za kimaendelea hasa uchumi na burudani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles