23.1 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Halotel Tanzania yatembelea kituo cha watoto cha Human Dreams

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel Tanzania imefanya ziara maalum katika kituo cha watoto cha Human Dreams Children Village, kinachojihusisha na kulea watoto yatima wenye ulemavu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo, ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za kampuni kutoa msaada na kusaidia jamii inayohitaji.

Wafanyakazi wa Halotel walijumuika na watoto katika kituo hicho kilichopo Kigamboni, jijini Dar es Salaam kutoa msaada wa vifaa mbalimbali, vikiwemo mahitaji muhimu ya kila siku kama vile vyakula, vifaa vya ndani pamoja na fedha.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Ofisa wa Mawasiliano na Uhusiano wa Halotel, Happy Mushi amesema wanatambua changamoto ambazo wanazipata watoto wenye ulemavu.

“Tunatambua changamoto ambazo watoto wenye ulemavu wanazipitia, na ni jukumu letu kama kampuni kuhakikisha kwamba tunawasaidia ili waweze kufikia ndoto zao. Tunatumaini msaada wetu utaleta mabadiliko chanya katika maisha ya watoto hawa,” amesema Happy.

Aidha viongozin wa kituo cha Human Dreams Children Village walionyesha furaha yao kwa ziara hiyo, wakisema kwamba msaada wa Halotel utawezesha kuboresha hali ya maisha ya watoto wao.

Amesema Halotel Tanzania inajivunia kuendelea kushiriki katika miradi ya kijamii, kwa lengo la kuboresha maisha ya Watanzania kupitia huduma bora za mawasiliano na shughuli za kijamii zinazolenga makundi yenye uhitaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles