28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Halotel Tanzania kugawa zawadi Kemkem Maonyesho ya Sabasaba

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Halotel Tanzania inayo furaha kubwa kutangaza kuwa itaweka kumbukumbu mpya kwenye Maonyesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (SabaSaba) mwaka huu kwa kugawa zawadi kemkem kwa wateja wake. Tukio hili limeanza rasmi Julai 28, ambapo wateja wote waliotembelea banda la Halotel walipata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali.

Leo, Halotel walizindua droo yao maalum ya kujishindia simu janja, ambapo mteja anaweza kujishindia zawadi nyingine nyingi pamoja na zawadi kuu ya Samsung Galaxy A14.

Katika maonyesho haya, Halotel pia inawapa wateja wake fursa ya kujifunza zaidi kuhusu bidhaa na huduma mpya, ikiwemo mtandao wa kasi wa 4G, vifurushi vya intaneti vya gharama nafuu, na suluhisho za kisasa za mawasiliano kwa biashara.

Droo hii iliendeshwa na msanii maarufu wa muziki, Elias Barnabas, maarufu kama Mopao Barnaba, ambaye aliwazawadia washindi wawili waliobahatika kushinda simu za Samsung Galaxy A14. Mshindi wa kwanza alikuwa, Veronica Maurusi na mshindi wa pili alikuwa Ibrahim Rashid.

Aidha, Halotel imewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kutembelea banda la Halotel na kushiriki katika bahati nasibu hii ya kipekee. Usikose nafasi ya kuwa mshindi!

“Usikose nafasi hii adhimu ya kujipatia zawadi na kujifunza zaidi kuhusu huduma bora za Halotel. Tunawahimiza wananchi wote kujitokeza kwa wingi kwenye maonyesho haya,” alisema mwakilishi wa Halotel.

Maonyesho ya SabaSaba yanaendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi na kampuni mbalimbali, na Halotel inajivunia kushiriki na kutoa huduma bora kwa wateja wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles