Na Iman Nathaniel, Dar es Salaam
KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Halotel kupitia huduma yake ya HaloPesa,imezindua huduma nyingine ya kujishindia zawadi mbalimbali iliyopewa jina la ‘Play & Win kwa wateja wake nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 27, 2021, jijini Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa HaloPesa, Magesa Wandwi, amesema Play& Win ni hatua nyingine ya ubunifu kutoka ya kufikisha thamani ya maisha ya wateja wake.
‘’Tuna uhakika kwamba wateja wa HaloPesa watafurahia huduma yetu na ambao bado hawajatumia HaloPesa watajiunga ili kufurahia huduma hii,”amesema.
Kwa upande wa mkuu wa huduma na mahusiano wa kwa wateja wa Dunia Investment ambaye ni mbia wa huduma ya hiyo,Kobus Schoeman, amesema kuwa michezo na burudani ni sehemu ya asili ya utamaduni wa Afrika ambapo kwa inagusa maisha.
Naye Ofisa wa bidhaa na masoko wa HaloPesa ,Roxana Kadio amesema kuwa katika kampeni hiyo mteja atapata halopointi za bure kulingana na aina ya miamala .