25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

HALMASHAURI ZATAKIWA KUNUNUA DAWA ZA VILUWILUWI

Na Benedict Liwenga-WHUSM


HALMASHAURI   zimetakiwa kuitikia wito wa kununua dawa za kuua viluwiluwi vya mbu wa malaria zilizoanza kuzalishwa   nchini   kukabiliana na   malaria.

Akzungumza na waandishi wa habari jana. Kaimu Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wa malaria cha Tanzania Biotech Products Limited kilichopo Kibaha, Samwel Mziray,  alisema dawa  hizo zinapaswa kununuliwa na kila halmashauri nchini kwa maagizo yaliyotolewa na Serikali.  

Alisema kiwanda hicho kinachomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 kilijengwa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa serikali katika kupambana na malaria nchini.

Hata hivyo alisema mpaka sasa mwitikio wa halmashauri umekua mdogo kwa sababu ni halmashauri mbili tu za Geita   na Mbogwe ndizo zimekwisha kununua dawa hizo.

“Lengo la Serikali kuja na mpango huu ni kupunguza vifo vinavyotokana  na malaria nchini na kupunguza gharama kubwa ya kununua dawa na vifaa tiba vya kupambana na malaria,” alisema Mziray.

Alisema   iwapo kama halmashauri zitanunua dawa hizo na kuzitumia, ugonjwa huo utapungua kwa kiasi kikubwa nchini na hivyo Serikali kuelekeza fedha zake katika shughuli za maendeleo.

Mziray alisema kwa Afrika, kiwanda hicho ni moja ya viwanda vilivyobahatika kujengwa Tanzania,  nia ya Serikali ikiwa ni kutokomeza   malaria kwa kuharibu mazalia ya mbu.

Meneja huyo alisema kiwanda hicho kitazalisha mbolea ya kibaiolojia (Bio fertilizer) siku zijazo lakini kwa sasa kiwanda kinazalisha dawa za aina mbili ambazo ni Bactivec na Griselesf ambazo hutumika   kunyunyuzia katika mazalia ya mbu.

“Niiombe Serikali iweze kutoa msukumo zaidi kwa halmashauri ambazo bado hazijanunua dawa hizi kukitumia kiwanda hiki kufikia malengo ikizingatiwa jamii inapoteza wapendwa wao kutokana na   malaria,” alisema Mziray.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles